Mkuu wa bunge la Libya anasema
kuwa watu kama 50 wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya balozi wa
Marekani mjini Benghazi juma lilopita.
Akizungumza na shirika la habari la Canada, CBS, Bwana Megaryef alisema anaamini wageni wenye uhusiano na Al-Qaeda walihusika.
Balozi wa Marekani, Chris Stevens, na Wamarekani wengine watatu, waliuwawa wakati guruneti lilipopiga ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi na kuwaka moto.
No comments:
Post a Comment