Thursday, September 27, 2012

Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?fuatilia habari hii kwa kina hapa uone jinsi ngudu walivyopitishwa kuendelea kula nnchi.

Salma Rashidi KIKWETE
Mwanaisha Halfani KIKWETE
Mohamed Mrisho KIKWETE
Ridhiwani Jakaya KIKWETE

Vita Rashidi Kawawa
Zainab Rashid Kawawa

Bayoum Awadhi KIGWANGALLA
Hamisi Andrea Kigwangalla

Saumu Mohamed BENDERA
Denis William BENDERA
Stanley J. BENDERA
Saum Mohamed BENDERA

William John MALECELA
Anne Kilango MALECELA

Lulu Abbas MTEMVU
Abbas MTEMVU

Sophia Mnyambi SIMBA
Ulanga Agathon SIMBA

Aisha Omar Kigoda
Abdallah Omari KIGODA

Wakati Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha kazi ya uteuzi wa wagombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali za chama hicho, vita kubwa inaonekana kuwa katika nafasi 10 za ujumbe wa Nec kwani mawaziri sita ni miongoini mwa wanachama 31 wa Bara watakaopamba vikali kupata nafasi hizo.
Hali ni hiyo pia kwa uopande wa Zanzibar kwani katika wanachama 28 wanaowania nafasi 10 za Nec Zanzibar, wapo mawaziri wanne.
Mbali na mawaziri sita nafasi 10 za Tanzania Bara pia  kuna wabunge watatu, mkuu wa wilaya mmoja na vigogo wawili wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Kwa upande wa Zanzibar wamo mawaziri wanne akiwamo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.
Mawaziri watakaochuana Bara ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. David Mathayo David; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge),  William Lukuvi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira; Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January Makamba.
Pia wamo Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama, Mbunge wa Iramba Magharibi na Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM, Mwigulu  Nchemba, wote ni wajumbe wa Kamati Kuu.
Wengine ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Sadrudin Bhanji; Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM),  Martine Shigela na Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama.
  Wamo pia Otieno Peter Baraka, Twalhata Ally Kakurwa, Godwin Emmanuel Kunambi, Innocent Mahendeki Nsena, Richard Hiza Tambwe, Anna John Magowa, Christopher Thomas Mullemwah, Salehe Mbwana Mhando,  Fadhili Emmanuel Nkurlu, Tumsifu Aaron Mwasamale, William John Malecela, Rashid Mrisho Kakozi, Dk. Luteni Kanali Kesi Athuman Mtambo, Nicholaus Daniel Haule na Nussura Gilbert Nzowa.
Wengine ni Hadija Uledi Faraji,  Dk. Hussain Abdulrehenan Hassan na Mwanamanga Juma Mwaduga, Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Blasio Msafiri na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson William Msome.
Kwa upande wa visiwani walioteuliwa kuwania nafasi hizo Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi; Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Abdallah Juma Sadallah, na Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee,
  Wengine ni  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kukenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mnyaa Mbarawa pia humo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Wengine ni Kidawa Hamid Saleh, Abdisalaam Issa Khatib,  Khadija Hassan Aboud, Abdalla Ali Hassan, Mohamed Ahmada Salum, Abdulhakim C. Chasama, Ali Mohamed Ali, Haji Makame Ali, Ibrahim Khamis Fataki, Moza Jaku Hassan, Nassir Ali Juma, Jecha Thabit Kombo, Khamis Mbeto Khamis,  Mohamed Hassan Moyo, Bhaguanji M. Mansuria Moudline C. Castico, Yakoub Khalfan Shaha, Rose Joel Mihambo, Ali Omar Mrisho na Mariam Omar Ali.

No comments:

Post a Comment