Wednesday, September 26, 2012

NIMEZIPATA PICHA ZA HOTELI YA KIFAHARI ILIYOTAJWA KUWA NAMBA 1 DUNIANI NA IPO TANZANIA, PICHA NDIO HIZI.toka millardayo.com

Hoteli inaitwa Singita Serengeti the Grumeti reserves Tanzania, na hii ni moja ya Lodge tano zilizochini ya hoteli hii, zote ziko mbalimbali kidogo na kiwango cha chini kabisa kulala kwa siku ni USD elfu moja na 50.
Nimeambiwa ukishaingia kwenye hoteli kuagiza kinywaji au chakula ni tani yako, pesa unayolipia kwa siku imejumuisha chakula pia na vinywaji pia.
Taarifa za uhakika ni kwamba kama wiki nne au tano zilizopita waigizaji mastaa wa dunia Angelina Jolie na Brad Pitt walifunga ndoa ya siri na yenye ulinzi kwenye hoteli hii ndani ya lodge ya Sasakwa, watu hawakutakiwa kusogelea wala kamera hazikutakiwa.
Miongoni mwa mastaa ambao mpaka sasa wameshafika kwenye hoteli hii ni pamoja na tajiri wa dunia Bill Gates na baadhi ya washindi wa Olympic 2012.
Lodge tano zilizochini ya hoteli hii ni Singita serengeti, The Grumeti reserves yenye Sasakwa lodge, Farufaru Lodge, Sabora Plains tented camp, Singita explore mobile tented and Serengeti house.
Mmiliki ni mmarekani Paul Tudor ambae ameshawahi kuwekwa kwenye list ya mabilionea katika jarida la Forbes na kwenye hii hoteli anashirikiana na Luke Bailes.
hapa chumbani.
Nimeambiwa hii hoteli imeibuka kuwa ya kwanza kwa ubora duniani katika list ya hoteli 100 zilizoshindanishwa.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Huduma ya farasi inapatikana pia.
.
Clouds Tv kama kawaida kwenye Exclusive interview na mmoja kati ya wasimamizi.
.
.
.
.
.
.
.
.
Wengi wa wateja wanasafirishwa na ndege kwenda kwenye hizo lodge na baada ya hapo ndio wanachukuliwa na magari.
Asante sana mybrother Simon Simalenga kwa picha.

No comments:

Post a Comment