Polisi wakilinda makaburi hayo ya siri |
Polisi na wataalamu wa
kuchunguza maiti wamepigwa na mshangao mkubwa baada ya kukosa kupata
chochote ndani ya makaburi ya siri yaliyogunduliwa katika eneo la Tana
River.
Polisi walipewa amri ya kufukua makaburi hayo
hii leo katika kijiji cha Ozhi ambako mapigano kati ya jamii za Orma na
Pokomo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu miamoja na kuwaacha maelfu
bila makao.Ingawa bwana Kamitu alisema kuwa hawakupata miili yoyote licha ya kuwa kulikuwepo na harufu mbaya ishara kwamba maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa.
Bwana Kamitu anasema kuna hofu kuwa wahalifu kutoka jamii ya Pokomo waliitoa hiyo miili kwenye makaburi hayo huku polisi wakisubiri kibali cha mahakama ili kuweza kuyafukua.
Polisi wamefahamisha BBC kuwa makaburi hayo yalikuwa tu na mguu mmoja wa kushoto wa mtu na wanashuku kuwa maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa na kupelekwa kwingineko.
Zaidi ya watu miamoja wamefariki katika mapigano kati ya jamii hizi mbili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa mwezi mmoja ulipita.
Makabiliano kati ya jamii hizo mbili yalianza katikati ya mwezi jana na kusababisha mashambulizi ya kuvizia na ya kulipiza kisasi.
chanzo bbc
No comments:
Post a Comment