Tuesday, September 25, 2012

Okwi, Sinta warushiana maneno mazito kweupe KIila mmoja anamshutumu mwenzake kwa kuandika magazetini



Emmanuel Okwi

STRAIKA namba moja wa Simba, Emmanuel Okwi ameweka bayana kwamba mwigizaji wa Bongo, Christine Sinta anajikomba kwake huku binti huyo naye akicharuka na kutamka mambo mazito.

Mchezaji huyo amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na maneno mengi yanayoenezwa na watu pamoja na msanii huyo kuwahi kunukuliwa akikiri kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.

Okwi kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook aliandika: "Habari mabibi na mabwana, napenda kuchukua nafasi hii kufafanua kinachoendelea baina yangu na Christine Sinta.
"Mambo mengi sana yameandikwa kwenye magazeti hata kwenye blogu yake kwamba tuna uhusiano wa kimapenzi kitu ambacho ni uongo mtupu. Nina imani kwamba mtanielewa ninachokisema.
"Imezidi mno, nilijaribu sana kupuuzia yaliyokuwa yanasemwa kuhusu sisi wawili lakini nadhani ni wakati mwafaka kwa nyie na kila mmoja kujua ukweli.
"Mimi sina uhusiano wa kimapenzi na yeye kama anavyodai, wala hakuna ukweli wowote kwa chochote kile anachokiandika kwenye mitandao, asanteni kwa sapoti yenu na Mungu awabariki," alimaliza Okwi.
Sinta aliiambia Mwanaspoti jana Jumatatu kwa njia ya simu akiwa Kampala,Uganda kuwa anamshangaa mchezaji huyo.
"Unajua mimi namwangalia sana Okwi na maneno yake namshangaa sana, anazungumza vitu vingi sana na kuandika kwenye facebook yake lakini mwisho wa siku anaishia kunipigia simu. Mimi wala siongei chochote.
Aachane na mimi.
"Simtaki. Hayo maneno anayoyasikia yanazungumzwa na magazeti ya udaku wala si tamko langu, sikuwahi kusema namtaka. Nawaheshimu sana Mwanaspoti ndiyo maana nimeamua kutoa ufafanuzi.
Nina mtu wangu siwezi kutembea na mwanasoka mimi, kiwango changu ni cha juu sana nimeshapita huko," alisema Sinta huku akitoa maneno machafu yanayoashiria jazba ambayo kimaadili hayafai kuchapishwa gazetini.
Sinta aliwahi kukiri kwamba urafiki wake na Okwi ulianzia Uganda tangu alipokuwa akisoma huko miezi ya hivi karibuni.
Okwi amejipatia umaarufu mkubwa nchini kutokana na umahiri wake kwenye soka akiwa na Simba na kila mechi amekuwa akifunga au kusababisha goli jambo ambalo limemfanya kukubalika na mashabiki.
Miaka ya nyuma, Sinta aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa Juma Nature wa kundi la Wanaume Halisi, mpaka msanii huyo akafikia hatua ya kumtungia wimbo alioupa jina la 'Inaniuma Sana'.

No comments:

Post a Comment