Ikiwa ni siku ya pili toka
mwandishi wa habari wa Channel Ten Daudi Mwangosi kuuwawa kwa bomu akiwa
kwenye mikono ya polisi Iringa, Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel
Nchimbi ameunda tume huru ya watu watano kwa ajili ya kuchunguza chanzo
cha kifo hicho.
Hiyo tume inaongozwa na jaji
mstaafu Stephen Kihema na itafanya kazi yake kwa siku 30 ambapo pamoja
na mambo mengine, inapaswa kuainisha ukubwa wa nguvu iliyotumika kumuua
mwandishi huyo, ichunguze kama upo uhasama kati ya Polisi na waandishi
wa habari mkoani Iringa, pia iangaliwe kama kweli ipo orodha ya
waandishi wa habari watatu waliopangwa kushughulikiwa na jeshi hilo.
Waziri Nchimbi ameahidi hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika kuhusika na kifo hicho bila kujali nafasi aliyonayo.
Kwenye line nyingine, namkariri
Nchimbi akisema “kuna maswali kama sita ambayo mimi sina majibu yake na
ningependa sana nipate majibu yake, nini chanzo cha kifo cha mwandishi
wa habari wa Iringa Daudi Mwangosi? nikiwa Waziri mwenye dhamana ya
usalama wa raia kwa sababu hiyo basi naunda kamati ya uchunguzi ya watu
watano”
Kuhusu msg iliyotumwa na Dr
Slaa kwa Mkuu wa jeshi la Polisi IGP Said Mwema kabla ya mwandishi
kuuwawa, naendelea kumkariri Waziri Nchimbi akisema “IGP Mwema
alitutumia hiyo msg viongozi wenzake, Dr Slaaa alimuandikia kwamba IGP
nasubiri simu yako wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha
kutakua na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea mjiandae kwenda
Mahakamani The Hague”
Kwenye nukuu nyingine Waziri
Nchimbi amesmea “nikiona mtu katuma msg ya namna hii kwa IGP alafu bado
yuko barabarani anaendelea kutembea, hajahojiwa, hajapelekwa Mahakamani
kwa kuandaa vurugu, ni jambo nalishangaa sana… kwa kweli ujumbe wangu ni
kwa watu wawili.. IGP namshangaa kwamba aliemtumia msg hiyo yuko
barabarani anatembea akiwa huru, pili namshangaa alietuma ujumbe huo
ambae ameona vifo vimetokea baada ya ujumbe wake bado hajajisalimisha
polisi”
No comments:
Post a Comment