CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya
Kikwete kuwasimamisha kazi vigogo wote wa Jeshi la Polisi, ambao
wamekuwa wakitoa taarifa tata kuhusu mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi,
kujiuzulu nyadhifa zao na kupisha uchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Mahusiano na
Habari wa chama hicho, John Mnyika, aliwataja vigogo hao wa polisi kuwa
ni Kamanda wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na RPC wa Iringa,
Michael Kamhanda, ambao katika nyakati tofauti walidai kuwa Mwangosi
alifikwa na mauti baada ya kuchoropoka kutoka kundi la wafuasi wa
CHADEMA na kukimbilia mikononi mwa polisi na ghafla kulitokea mlipuko wa
bomu la machozi uliosababisha kifo cha mwandishi huyo jambo ambalo sio
la kweli.
Mnyika alisema maneno hayo yanatofautiana na ukweli na kuyaita kuwa ni
ya uongo, ikizingatiwa kwamba picha mbalimbali zimeonesha kilichotokea,
ikiwemo waandishi waliokuwemo eneo la tukio kutoa ushuhuda wao.
Kutokana na hali hiyo, Mnyika alisema ipo haja ya vigogo hao kung’oka na kupisha uchunguzi ili uweze kufanyika kwa haki.
Kwa
mujibu wa Mnyika, polisi imekuwa na tabia ya kukamata raia wanaokuwa
eneo la tukio pindi kunapotokea mauaji kama hayo, hivyo ni wakati sasa
wa polisi wanaoonekana katika picha wakimshambulia marehemu Mwangosi nao
kukamatwa.
Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi lisitumie vibaya fedha za walipa kodi kwa kuchunguza nani alihusika na mauaji hayo, wakati wauaji wanaonekana wazi kwenye picha, hivyo kinachotakiwa na wao kuhojiwa nani aliwaamuru kufanya mauaji hayo ya kinyama.
Alisema uchunguzi huo hauwezi kufanywa na polisi na badala yake unatakiwa kufanywa na chombo huru cha mahakama ambapo rais anapaswa kutumia sheria ya vifo kifungu cha tatu na kuwezesha kuundwa kwa chombo cha kimahakama ili kuweze kufanyika uchunguzi huru wa nyuma ya pazia mambo yote yaliyotokea na ukweli kuweza kudhihirika.
Pia Mnyika alitumia fursa hiyo kukanusha kuwa chama chao kimekuwa kikikaidi utawala wa sheria.
“Kuna ushahidi tosha wa matukio ya CHADEMA kuwa katika mikutano ya ndani ya chama ambapo polisi ndio walifika na kufyatua mabomu… hata pale watu walipoamua kutawanyika waliendelea kufyatua mabomu hayo hadi ndani ya ofisi zao,” alisema na kuongeza kuwa polisi wanaonesha wazi kuwa ndio wenye vurugu.
Alisema kama kweli polisi ilikuwa na dhamira ya kweli ya kuzuia maandamano ya CHADEMA kwa kisingizio cha sensa, ingemkamata Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Khalid Mohamed Bilal, akiwa amezindua mkutano wa hadhara Bububu ambao wala haukutawanywa na polisi kama ilivyokuwa kwa chama chao ambao wao walikuwa katika mkutano wa ndani.
Katika hatua nyingine, Mnyika amewataka wanachama wao kuchukua tahadhari hasa baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa kutoa taarifa kuwa Chama Cha Mapinduzi kinahusika na kuingiza silaha za kivita na kuwafundisha vijana mafunzo ya kivita kwenye makambi, ambapo wanataka kuigeuzia kibao CHADEMA na kupandikiza watu wao kwenye operesheni za chama hicho ili waonekane ndio wakorofi.
Kutokana na hali hiyo, amewataka viongozi na wanachama watakaokuwa kwenye operesheni hizo kuchukua hatua pale watakapowatilia shaka watu hao.
Pamoja na hilo, Mnyika alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesitisha ziara yake nchini Marekani na alikuwa akitarajiwa kuwasili jana ili kusimamia na kuendeleza mashauriano na baadae kuja na tamko la hatua gani wameamua kuzichukua endapo serikali haitaweza kushughulikia maagizo ambayo wameyatoa awali.

No comments:
Post a Comment