Sunday, September 30, 2012

Liverpool yaifunza Norwich baada yakuifunga 5-2


                                 Suarez akifunga moja ya mabao matatu aliyofunga jana
Mshambuliaji matata wa Liverpool, Luis Suarez amefunga magoli matatu kati ya matano dhidi ya mawili ya Norwich, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa timu ya Liverpool katika msimu huu wa ligi kuu ya England.
Suarez alifunga goli la pili akiwa nje ya eneo la hatari baada ya kumiliki mpira akielekea lango la Norwich.
Suarez alifunga bao la tatu baada ya ushirikiano mzuri na Nuri Sahin.
Nohodha Steven Gerrard alishindilia msumari wa mwisho katika jeneza la Norwich kwa kufunga bao la tano na kuifanya timu hiyo kuangukia sasa nafasi ya 14 kati ya timu 20 za ligi kuu ya premier.
Kileleni wapo Chelsea wenye pointi 16.

No comments:

Post a Comment