watoto |
Takriban watoto milioni 6.9
walifariki kabla ya kufikisha miaka mitano mwaka jana ikilinganishwa na
vifo milioni 12 vya watoto wachanga vilivyotokea mwaka 1990. Takriban
watoto elfu kumi na tisa walifariki mwaka 2011.
Kwa mujibu wa shirika la kuwahudumia watoto la
Umoja wa mataifa Unicef, sababu mojawapo ya kupungua kwa vifo ni nchi
maskini kutajirika.
Nchi ambazo idadi ilipungua sana ni zile ambazo zilipata msaada mwingi kutoka nje.
"ukiangalia, nchi ambazo idadi ya vifo imepungua sana mfano Jamuhuri ya watu wa Lao, Timor na Liberia
ambazo ni nchi tatu za kwanza katika orodha ya nchi ambako idadi ya vifo ilipungua, nadhani kwa nchi hizi zote msaada unaotoka nje umechangia pakubwa jambo hilo,'' alisema mkurugenzi mkuu wa shirika la Unicef nchini Uingereza, David Bull.
ambazo ni nchi tatu za kwanza katika orodha ya nchi ambako idadi ya vifo ilipungua, nadhani kwa nchi hizi zote msaada unaotoka nje umechangia pakubwa jambo hilo,'' alisema mkurugenzi mkuu wa shirika la Unicef nchini Uingereza, David Bull.
Juhudi zinazolenga magonjwa ya kuambukizana kama
Ukambi, zimepunguza vifo duniani kutoka vifo vya watoto laki tano mwaka
2000 hadi vifo laki moja mwaka 2011.
Mwaka jana nusu ya vifo vya watoto wachanga
duniani vilitokea katika nchi tano pekee kulingana na Unicef. Hizi nchi
ni pamoja na India, Nigeria, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Pakistan
na China.
Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chad,
Somalia, Mali, Cameroon na Burkina Faso idadi ya vifo vya watoto
iliongezeka kwa vifo 10,000 au zaidi mnamo mwaka 2011 ikilinganishwa na
mwaka 1990.
Karibu vifo hivyo vyote vilichangiwa na ugonjwa
wa Malaria kwa watoto walio chini ya miaka mitano katika nchi za Kusini
mwa jangwa la Sahara mwaka jana kwa mujibu wa shirika hilo. Mizozo pia
ilichangia huku ugonjwa wa kichomi na tatizo la kuharisha vile vile nayo
yakichangia vifo hivyo.
No comments:
Post a Comment