Alisema katika kikao hicho watajadili kauli za awali za polisi kuhusu tukio hilo, kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Tendwa, Waziri wa Mambo wa Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na mustakali wa uhuru wa vyombo vya habari.
Pia alisema watajadili utendaji kazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambalo alieleza sasa linatumika kama kipeperushi cha serikali.
“CHADEMA hatutegemei TBC kutengeneza habari, kwani baada ya kuondoka Tido Mhando sasa imekuwa kipeperushi cha serikali. tutajadili mahusiano yetu na TBC na kutoa tamko zito kuhusu hatma yetu na TBC.
“Hakuna ugomvi na waandishi na wapigapicha wa TBC, kwani tunajua wao wanatumwa, bali uongozi. Tukio hili limetokea wao wanapindisha ukweli, wangekuwa na nia nzuri na busara wasingechukua habari za upande mmoja,” alisema.
CHADEMA sio chama cha mfukoni, na hatua zozote za kuzima vuguvugu la Mabadiliko hazitawezekana.Tutaendelea kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali propaganda zinazofanywa na Serikali dhidi yetu ili kuleta mabadiliko ya kweli.Dr.slaa
No comments:
Post a Comment