David silver |
David Silva ametia saini mkataba
mpya wa miaka mitano kuendelea kucheza soka katika klabu ya Manchester
City, na atasalia katika uwanja wa Etihad angalau hadi mwaka 2017.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Uhispania, mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na
timu hiyo kutoka Valencia mwaka 2010, na alishindwa kucheza katika mechi
mbili tu tangu alipojiunga na City, ambao waliibuka mabingwa wa ligi
kuu ya Premier msimu uliopita, na ukiwa ndio ushindi wao wa kwanza tangu
mwaka 1968.
Mchezaji huyo alikuwa amehusishwa na gumzo kwamba
alikuwa na mipango ya kurudi Uhispania, lakini amesisitiza atakuwa radhi
kuendelea kucheza soka nchini Uingereza."Ninajihisi nimo katika hali ya furaha katika klabu, na hayo ikiwa ni pamoja na wakazi wa mji huyo," ameelezea kupitia tovuti ya club yao leo hii
No comments:
Post a Comment