John Terry ameadhibiwa na chama
cha kandanda cha England, FA, asicheze mechi nne, na vile vile alipe
faini ya pauni 220,000, kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi
ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand. Chama cha FA kilithibitisha Terry alifanya makosa hayo, baada ya kusikiliza kesi dhidi yake kwa kipindi cha siku nne. Msemaji
wa John Terry alisema mchezaji huyo "alisikitishwa" na hatua ya FA, kwa
kuamua tofauti, kinyume na mahakama, ambayo awali ilisema hana makosa.
Mwezi
Julai, mahakama ya Westminster mjini London ilipitisha uamuzi kwamba
mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 31, hakufanya kosa hilo, la kutumia
matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand.
Hata hivyo wengi watajiuliza kwa nini adhabu dhidi ya Terry ni nyepesi mno, ikilinganishwa na ile iliyopitishwa dhdi ya mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez mwaka jana. Terry ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mara tu atakapopokea maelezo ya adhabu hiyo kupitia maandishi. Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi Terry atakapopata nafasi ya kuamua atafanya nini.

Taarifa
kutoka klabu yake ya Chelsea iliongezea: "Klabu ya Chelsea inafahamu
vyema uamuzi uliopitishwa, na inaheshimu uamuzi huo uliotolewa leo na
chama cha FA kumhusu John Terry."
No comments:
Post a Comment