Kikosi cha Simba leo |
SIMBA SC imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
jioni hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo,
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na
Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Mrisho Ngassa dakika
ya 36 akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, ambayo tayari ilikuwa na mwelekeo wa
kutinga nyavuni.
Lyon walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na
Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi
cha pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba
iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffo aliifungia
timu yake bao la kuhitimisha ushindi
kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe,
Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/
Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.
African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi Manzi, Sunday Bakari, Benedictor
Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa, Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob
massawe na Yussuf Mlipili.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na
Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier
Kavumbangu na Stefano Mwasyika.
Kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC
ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey
Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao/Jabir Aziz, John Bocco,
Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo
dakika ya 41 liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila
kufungana na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.
Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya
1-1 na JKT Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga
Ruvu Shooting mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment