TAARIFA KWA WANAROMBO WOTE POPOTE PALE WALIPO DUNIANI HII INAWAHUSU SANA PLEASE SHOW UP!!
Jimbo
la Rombo limekuwa na wawekezaji wa ndani na nje pamoja na
wafanyabiashara wakubwa na wadogo lakini wamekuwa wakiwekeza nje ya
Jimbo na hivyo tatizo la Ajira kwa vijana wa Rombo limeendelea kukua
kila siku. Kama nilivyoahidi mwaka 2010 kwenye kampeni tayari wawekezaji
wameanza kurudi kuwekeza Rombo na wengine watarudi kuwekeza Rombo.
Mfano ni kiwanda cha Juice na Maji Safi cha SEQUA ambacho kimeanza na
uzalishaji wa Maji ya kunywa na Juice zitaanza kutengenezwa hivi
karibuni. Lengo ni kuwapa vijana Ajira pamoja na kukuza pato la wakulima
wa Matunda. Nitoe Wito kwa wana-Rombo kuanza kulima matunda ya aina
mbalimbali kwa wingi ili waweze kukidhi makitaji ya kiwanda hicho ambapo
kila siku yatahitajika matunda kati ya tani 5-10.
Pili jana
nimezindua kiwanda cha mikate kinachomilikiwa na Tumaini Center ambapo
kina uwezo wa kuzalisha mikate 250 kwa saa moja. Tumaini Center ni kituo
cha kuwasaidia watoto Yatima kupata Elimu na kwa sasa kina watoto zaidi
ya 350 ambapo wapo kwenye level mbalimbali za Elimu kuanzia Primary
hadi Chuo kikuu. Nimewaahidi 5million kutoka kwenye CDCF ili ziweze
kuwasaidia japo wanafunzi kadhaa kupata elimu hiyo kwa kuwa kituo hiki
kimekuwa kikijiendesha kwa miradi yao midogo midogo. Natoa wito kwa
Wana-Rombo popote walipo kukisaidia kituo hiki kwa hali na mali ili
kiweze kuendelea kutekeleza majukumu yake mazuri kwa ustawi wa Jamii
yetu. Kwa wale wasiojua namna ya kukichangia naomba tuwasiliane kwa
maelekezo zaidi.
Haya yote nitayasisitiza kwenye Mikutano yangu
ya M4C nitakayoianzisha leo tarehe 20-09-2012 hapa Rombo na kumalizika
tarehe 2-10-2012.
Leo nitaanzia kata ya Najarareha ambapo pamoja na mambo mengine nitazindua matawi na ofisi kadhaa za Chama wilayani hapa.
Ahsanteni, M4C.
Joseph R. Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA)
No comments:
Post a Comment