Magwanda ya mabomu ya kujilipua |
Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda
yenye mabomu ya kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa
zitumike kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi.
Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, ambapo watu 76 waliuawa
No comments:
Post a Comment