Stori mpya ni kwamba kocha wa Man U Sir Alex Ferguson amekiri kupitia gazeti la Mirror UK kwamba Usain Bolt ambae ni shabiki mkubwa wa Manchester united atapata nafasi ya kuichezea Man U kama mchezaji kwenye mechi ya kirafiki na Real Madrid siku zijazo.
Tayari mpaka sasa Bolt ameshatembelea uwanja wa mazoezi wa Man United na kukutana na wachezaji wa club hiyo, na sasa imethibitika kwamba jamaa atapewa namba kwenye mechi ya Man U na Real Madrid ili kuangaliwa uwezo wake.
No comments:
Post a Comment