WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewavua madaraka
wakurugenzi sita wa Halmashauri za Wilaya kwa kushindwa kusimamia
rasilimali watu, fedha na kutowajibika.
Kutokana na hatua hiyo,
Waziri Mkuu Pinda amewateua watu sita kukaimu nafasi hizo na wakurugenzi
wapya 14 huku akiwahamisha wakurugenzi 27 kutoka katika vituo vyao vya
kazi kwa sababu mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) Hawa Ghasia, alisema wakurugenzi hao walivuliwa madaraka kwa
kushindwa kusimamia rasilimali watu na fedha, kusababisha halmashauri
kupata hati chafu na uzembe.
Aliwataja wakurugenzi hao waliovuliwa
madaraka kuwa ni Willy Njau (Mwanga), Mpangalukela Tatala (Geita),
Theonest Nyamhanga (Kishapu), Eden Munisi (Morogoro), Mhando Senyagwa
(Kyela) na Nicholaus Kileka (Ngorongoro).
Pia alisema Serikali
haitasita kuchukua hatua pale inapobidi ili kuboresha utendaji, na
kwamba wengine tayari wana kesi na si busara kuwe na mtu anayekaimu
zaidi ya miaka mitatu.
Pia alisema hatua za kinidhamu bado
zinaendelea na kwamba baadhi ya wakurugenzi hao tayari wamewafikisha
kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya
hatua zaidi.
Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya walioteuliwa
kujaza nafasi hizo kuwa ni Abdalah Kidwanka (Geita), Rutius Bilakwata
(Kishapu), Naomi Nko (Magu ), Abdalah Mfaume (Kyela), Twalib Mbasha
(Monduli), Henry Ruyagu (Urambo), Adam Mgoyi (Mbarali) na Estomih
Chang’a (Mpanda).
Wamo pia Leti Shuma (Mwanga), Mohamed Maje
(Namtumbo) Fulgency Mponji (Moshi), Robert Nehata (Tunduru), Isabela
Chilumba (Kahama), Fikiri Malembeka (Sengerema), Paul Malala (Njombe) na
Nasib Mbaga (Biharamulo).
Wakurugenzi wanaohamishwa ili kujaza
vituo wazi ni Bibie Mnyamagola (Kongwa), Daudi Mayeji (Kilindi), Protace
Magayane (Nkasi), Saada Mwaruka (Mkuranga), Sipora Liana(Tabora
Manispaa), Hadija Makuwani (Wilaya ya Tabora), Doroth Rwiza (Kasulu).
Wengine
ni Kelvin Makonda (Manispaa ya Lindi), Pudenciana Kisaka (Iringa), Tina
Sekambo (Makambako), Beatrice Dominick (Masasi), Gladyness Ndyamvuye
(Bukoba), Nathan Mshana (Ngorongoro), Cornel Ngudungi (Ngara), Mohamed
Mkupete (Mtwara Manispaa), Dk Koroine Ole Kuney (Misungwi).
Wamo
pia Ephraem Ole Nguyaine (Rorya), Goody Pamba (Igunga), Fidelis Lumato
(Ludewa), Athuman (Tarime) na Ahmad Sawa (Musoma Manispaa).
Waliohamishwa
kwenda kwenye halmashauri mpya ni Magreth Nakainga (Geita), Eliza Bwana
(Bariadi), Zuberi Mbyana, Ilemela Manispaa (Biharamulo), Mohamed
Nanyanje (Masasi), Erica Musika (Kahama), Imelda Ishuza (Busokelo).
Chanzo -Mwananchi
No comments:
Post a Comment