Maafisa wa utawala mjini Cairo,
wameamuru kukamatwa kwa wakiristu saba wa kikopti raia wa Misri
wanaosihi nchini Marekani kwa kuhusika na utengezaji wa filamu iliyozua
ghadhabu miongoni mwa waisilamu wengi kote duniani.
Filamu hiyo ambayo inamkejeli mtume Muhammad ilizua ghasia na kero katika mataifa ya kiisilamu kwa namna ilivyomdhihaki Mtume.Kibali cha kumkamata mchungaji Terry Jones nchini Marekani kimetolewa.
Mwanamke mmoja na wanaume saba akiwemo Jones, wanatuhumiwa kwa kuitusi dini ya kiisilamu na kuchochea ghasia za kidini , kwa mujibu wa taarifa za mwendesha mkuu wa mashtaka.
Taarifa hiyo ilisema kuwa shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, watafahamishwa kuhusu vibali hivyo.
Ombi pia litatolewa kwa maafisa wa kisheria nchini Marekani. Inaarifiwa kuwa ikiwa wote waliotuhumiwa watapatikana na hatia huenda
tutawaletea taarifa zaidi kadri tutakapopata habari zaidi
No comments:
Post a Comment