Arsenal 6-1 Southamton
Arsenal ilionyesha mchezo safi
uliojaa mashambulizi na kuwafanya wapate mabao matatu katika dakika saba
ya kipindi cha kwanza wa mechi kati yao na Southampton.
Jos Hooiveld wa Southampton aliipatia Arsenal
bao la kwanza baada ya kujifunga mwenyewe kabla ya Lukas Podolski
kuvurumisha mkwaju mkali toka umbali wa yadi 25 na kufanya mambo kuwa
2-0.Kiungu Gervinho aliwapa vijana wa Arsene Wenger bao la tatu kabla ya Nathaniel Clyne wa Southampton kujifunga mwenyewe.
Hata hivyo Danny Fox alijitahidi na kuwapa wagine bao la kufutia machozi.
Baada ya kutoka mapumzikoni, mwamba Gervinho aliipa Arsenal bao la tano kabla ya Theo Walcott kufunga la sita mara tu baada ya kuingizwa uwanjani.
Licha ya kucheza mechi nne Southampton hadi sasa bado haijapata pointi yeyote na inavuta mkia katika ligi hiyo ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment