Msimamo wa CHADEMA
Wakati hayo yakijiri, CHADEMA kwa upande wake, kimetoa msimamo wa
kukataa kwanza, kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nchimbi
kuchunguza mauaji ya Mwangosi huko Iringa, lakini pia kinakusudia
kuwafungulia mashitaka ya mauaji makanda wa polisi wa mikoa ya Morogoro
na Iringa.
Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari jana mjini Morogoro,
Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene aliongeza kufikishwa mahakamani
kwa askari mmoja anayetuhumiwa kumuua Mwangosi hakuwezi kumaliza kiu ya
wapenda haki, akidai kuwa watuhumiwa wengine bado wanatamba mitaani.
“Uamuzi wa Kamati Kuu iliyokaa karibuni ni kwamba RPC wa Iringa,
Michael Kamuhanda akamatwe na afikishwe mahakamani kwa tuhuma za mauaji
ya Mwangosi, kwa sababu yeye ndiye alikuwa akiongoza operesheni wakati
polisi wanafanya mauaji hayo, alikuwa field.
“Lakini pia CHADEMA tunasema maaskari wote wanaoonekana kwenye picha
wakati Mwangosi anakamatwa, kupigwa na kuuwawa ni watuhumiwa wanapaswa
kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mauaji, chini ya hapo ni
kuwahadaa wapenda haki Tanzania na duniani kote ambao sasa wanaanza
kuiangalia Tanzania kwa jicho la aina yake kutokana na mauaji
yanayofanya na vyombo vya dola,” alisema Makene.
No comments:
Post a Comment