Leo jioni hii mh. Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa arusha mjini amefanya mkutano mkubwa hapa mjini moshi akishirikiana na meya wa manispaa ya moshi pamoja na madiwani wa chadema mjini hapa,mkutano huo ulifanyika kata ya mji mwema na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji wa manispaa ya moshi,
Pamoja na kuelezea uma huo kwa habari ya m4c pia lema alitumia mkutano huo kuelezea mgogoro wao na TBC hivyo kuwataka wakazi wa Moshi kutokuangalia hiyo television akiita kipeperushi cha ccm.Pia katika mkutano huo meya wa manispaa hiyo alitumia muda mwingi kumshambulia mkuu wa mkoa wa kilimanjaro kwa madai anaendesha kampeni za kuichafua CHADEMA makusudi kwa kuwazushia madiwani wa chama hicho kwamba wamepanga safari ya kifisadi kwenda kigali Rwanda.
Akitoa ufafanuzi wa tuhuma hiyo mh.jafari alifafanua kwamba wamepeleka mapendekezo hayo ya safari yao kwa waziri mkuu na bado hawajafikia muafaka wakweda na pia waziri mkuu hajatoa taarifa yoyote kwao kama pingamizi la bageti ya safari yao ya mafunzo na aliongeza kwamba katika safari hiyo ya siku7,siku nne hawatalipwa posho ambazo ni stahili zao ila wametoa kama mchango wao kwa manispaa na pia watalipwa siku tatu pekee.
Hata hivyo alielezea mafanikio yao tangu waingie madarakani wameongeza mapato kutoka 1.8bilion hadi 2.5bilioni kwa kudhibiti mianya ya rushwa iliyokuwa inatumiwa na wenzao wa ccm kujinufaisha biafsi,na alifafanua pia barabara nyingi zinazojengwa kwa sasa katika manispaa ya moshi ni juhudi za makusudi za madiwani wa chadema kufuatilia kwa karibu miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment