Saturday, September 15, 2012

Taarifa kwa umma toka BAVICHA ARUSHA

Ndugu waandishi wa habari,na Watanzania kwa Ujumla Wake

Hivi karibuni kwa zaidin ya mwezi na nusu sasa,kumejitokeza vijana wanaopita kwenye maeneo mbalimbali katika mji wa Arusha,wakitukana na kukikashifu chama chetu cha CHADEMA,matusi na kashfa hizi ni matokeo ya ripoti ambayo iliandaliwa na vijana watano wasomi wa chuo kikuu,waliotumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Malongo Magesa.Itakumbukwa kuwa Mkuu huyu wa mkoa wa Arusha aliletwa Arusha kwa sababu maalum,na moja ya sababu hizo ni kukidhoofisha CHADEMA,hivyo aliunda kikosi kazi hicho ambacho hata hivyo miongoni mwa vijana hao watano watatu ni vijana wangu,walizunguka Arusha,na kumletea ripoti MBOVU ambayo kwa UPOFU wake naye ameifanyia kazi,moja ya ushauri waliompa ni kuwatumia wanachama wa CHADEMA kuwatukana Viongozi wao na chama,hivyo Mkuu wa mkoa pamoja na Meya Feki wa Kichina,wakawarubuni vijana wawili wanachama wa CHADEMA ambao ni Niko na Kiyeuyeu.Vijana hawa Niko Na Kiyeuyeu ambao wanalipwa na M
kuu wa Mkoa pamoja na Meya wa Kichina,wamepewa pikipiki pamoja na Tshs 20,000 kila siku kwa kazi hiyo ya siasa chafu.Tunatoa Rai wa wakazi wote wa Arusha kuwapuuza Vijana hawa ambao njaa zinawasumbua hadi kufikia kujisaliti wenyewe.
BAVICHA mkoa wa Arusha tunalaani aina hii ya siasa,na tunamtaka mkuu wa Mkoa aache kutumia ofisi ya umma kwa maslahi ya ccm vinginevyo aachie ofisi ya Umma.Tunatambua kuwa mkuu wa Mkoa ana majukumu yake lakini Bwana Malongo Magesa amekuwa akiingilia utendaji wa Halimashauri ya manispaa ya Arusha,na kuwa kama Mkurugenzi,hivi karibuni alizuia Tenda ya kukusanya ushuru wa Mabango,kwa kuwa mzabuni aliyeshinda sio chaguo lake na badala yake akataka kampuni ya ndugu yake ndio ipewe Tenda wakati imetender kwa hela ndogo zaidi.
Tangu ateuliwe kushika wadhifa huu huyu RC amekuwa Kituko hapa Arusha,ameunda zaidi ya Tume tatu kuchunguza ubadhirifu ulio wazi wa Halmashauri ya manispaa ya Arusha,na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa huku tume hizo zikiwa zimetumia mamilioni ya walipa kodi maskini wa Arusha
BAVICHA tunamtaka afanye yafuatayo
1.Aache mara moja kutukana CHADEMA,na Viongozi wake,vinginevyo tutatangaza mgogoro naye
2.Aeleze umma wa Arusha juu ya Ripoti tatu za tume alizounda za kuchunguza ubadhirifu mkubwa katika Halimashauri ya manispaa ya Arusha,aeleze hatua gani alichukua
3.Achague kuwa Mkuu wa mkoa au Mkurugenzi
  ……………………..
Nanyaro Ephata
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Arusha
14/9/2012

No comments:

Post a Comment