Monday, September 24, 2012

ARUSHA KWA CHAFUKA NI USIKU WA KUAMKIA LEO

MORANI
 Mapigano makubwa kati ya wamasai na wameru yametokea usiku wakuamkia leo katika mpaka wa wilaya ya arumeru na longido,waarusha hao wenye hasira kali wanaoishi katika maeneo hayo ya wamasai walijikuta katika wakati mgumu wakati walipovamiwa ghafla usiku na inasemekana maboma kumi na mbili yameharibiwa vibaya na kuchomwa moto wakati ikiripotiwa watu kumi na mbili kujeruhiwa na kulazwa hospital ya wilaya,chanzo cha vurugu hizo bado hakijawekwa wazi vizuri wengine wakidai ni matatizo ya mipaka na maeneo ya malisho.
Wakati huo huo mkuu wa wilaya ya arumeru amesema wapo katika kikao muda huu karibu na eneo la tukio wakijadili jinsi yakukutanisha hizo pande mbili kwa ajili ya mazungumzo ya amani yakutatua mzozo huo ili mapigano yasiendelee.
Katika hatua nyingine inasemekana kila upande umeaandaa morani wakutosha ili kukabiliana na wenzao,upande wa meru unadaiwa kuwa na morani zaidi ya elfu tano na upande wa lngido unadaiwa pia kuwa na zaidi ya morani elfu tatu wakiwa na silaha za jadi tayari kabisa kwa mapambano.
tutaendelea kuwataarifu kila wakati tutakapopata habari mpya.
 

Wakati huo huo mkoani arusha mapema leo wanafunzi wa shule kongwe ya ilboru walifanya maandamano ya amani kwenda kwa mkuu wa mkoa kupeleka malalamiko yao mbalimbali juu ya mkuu wa shule anayedaiwa kuendesha shule hiyo jinsi apendavyo,pamoja na mambo mengine wanamtuhumu kwa kuwapa adhabu ambazo siyo za kawaida na kuwatoza faini za ajabu ajabu pindi wanapokosea na pia wamemtuhumu mkuu huyo kwa kuwaamisha walimu wao wenye uwezo mzuri kwa sababu za chuki zake binafsi.
mkuu wa mkoa akiwapokea aliwapongeza kwa hatua yao yakuandamana kwa amani na busara waliyotumia kuzungumza nae na kuahidi kufanyia kazi madai yao mapema iwezekanavyo ikiwa ni kufika shuleni hapo mapema na kuzungumza na pande zote mbili ili kutatua kero zao.

No comments:

Post a Comment