Sunday, October 20, 2013

WANAVYOWEZA KUIBA PESA KUPITIA MITANDAO YA SIMU

Kumetokea matukio kadhaa ya wizi kwa njia ya mtandao unaohusisha simu za mikononi katika utoaji wa fedha ingawa pesa nyingi zimetolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa kampuni za simu .


Tukio kubwa sana ni lile la kampuni moja kupoteza karibu bil 2.5 kwa mkupuo , ambapo walihusika wafanyakazi zaidi ya 5 huku mmoja wao akiwa ameacha kazi kabla ya tukio nitaeleza tukio hili kwa ufupi .

Hii kampuni haina tabia ya ufanya utaratibu wa kufuta rekodi za mtu aliyeacha kazi ndani ya muda mfupi haswa zile taarifa zake za kuingia kwenye kompyuta au anapotaka kuingia kwenye database na program nyingine za kiofisi .

Kilichotokea huyu kijana alivyoacha kazi , wenzake wakajua hivyo walijua kuna taarifa Fulani zimeachwa kwahiyo wakafanya utaratibu wa kufanya recovery ya password za huyu kijana aliyeacha kazi .

Password zilipatikana zote kwa ushirikiano wa kijana mwingine wa kitengo cha Tehama , kwahiyo wakaingia kwenye kompyuta ya huyu kijana aliyeacha kazi na kutengeneza wakala feki wa kutoa fedha , wakafungua zaidi ya 10 halafu wakaweka watu wao .

Wakaanza kutoa fedha kupitia hao wakala feki , kilichofanya washtukiwe ni kitendo cha kutaka kuhamisha zaidi ya mil 400 kwenda kwenye akaunti ya mmoja wao ndio hapo benki walipopiga simu kwenye kampuni hiyo ili kupata taarifa zaidi kwa bahati nzuri alipokea mtu wao , kesho yake benki ikapiga tena ndipo mwenzao hakuwepo , ndipo mchezo wao uliishia hapo walikamatwa lakini sasa wako nje sijui kesi yao iliishia wapi .

………………………………………………………………………………………..

Siku nyingine mfanyakazi mmoja wa kampuni ya simu alienda kwa dada mmoja kuomba namba yake ya uwakala akamwambia atamwingizia hela kiasi cha mil 1 kila siku kwa siku 3 yeye achukue laki 3 kwa kila hamisho .

Huyu mfanyakazi aliwasiliana na mawakala zaidi ya 50 kwa makubaliano hayo , kumbe huyu mfanyakazi alikuwa anafanya taratibu za kuacha kazi na kweli aliacha kazi akaenda kufuata zile fedha .

Kampuni ya simu ikashtuka hela zimehamishwa kwenda kwa mawakala hao na mfanyakazi ameacha kazi , walikuwa wameshachelewa sana , waliopata shida ni mawakala kwa kufungiwa huduma zao wengine kupelekwa polisi .

……………………………………………………………………………………..

Ukiwa unatoa huduma za uwakala wa kutoa fedha basi usipende kuzoeana sana na watu , kama unapenda sikiliza kisa hiki .

Mtu mmoja alizoeana na wakala Fulani kiasi kwamba aliweza kujua hata bosa wa yule wakala majina yake na namba zake za simu na hata vitu vingingine vidogo vidogo .

Siku moja huyu jamaa kwa kutumia program ya kompyuta akamwandikia huyu wakala sms . NAOMBA UTUME KIASI CHA LAKI 4 KWENYE NO 98686 JINA LAKE NI SSSS .Wakala kuangalia namba ni ya bosi wake kweli hakutaka kuhakiki hiyo sms vizuri yeye akahamisha hela akaibiwa .

Siku ya pili huyu mhalifu alienda kwa mtu mwingine kwa kutumia hiyo program akaandika ujumbe wa kutoa fedha  kiasi cha laki 4 ,wakala kuona sms akajua kweli yule mtu katoa hela kampa mhalifu hela kumbe ile ilikuwa sms tu , siku nyingine akajifunza mtu akitoa hela hakikisha nae anapokea sms ya kuthibitisha kutoa hela .

3 comments: