Saturday, September 8, 2012

Historia ya Paralympics-OLYMPIC YA WALEMAVU


 

Ulikua mwaka 1948, hospitali iliyo nje kidogo ya mji mkuu wa London ilishuhudia mwanzo wa vuguvugu la mashindano ya walemavu, baada ya daktari aliyekimbia utawala wa Nazi nchini Ujeremani mwenye asili ya Kiyahudi kujaribu kubadili maisha ya wagonjwa walioathiriwa na majeraha ya uti wa mgongo -- na hivyo kuwatia moyo washiriki michezo.  Michezo ya kwanza iliyojulikana kama "Stoke Mandeville Games" ilipangwa mwaka 1948 ili ifanyike sambamba na mashindano ya mwaka huo yaliyofanyika nchini Uingereza.  Jina Mandeville ni la Hospitali ya huko Buckinghamshire ambako Prof. Ludwig Guttmann aliongoza juhudi zake za tiba ya kiakili kwa wagonjwa wa uti wa mgongo walioshiriki michezo ya mwaka huo, wakiwa wanaume 14 na wanawake 2 walioshiriki wakiwa ndani ya magari ya walemavu na kushiriki mashindano ya kulenga mishale.  Daniel Diass muogeleaji mlemavu  Wengi wao walikua ni wanajeshi waliojeruhiwa katika vita vikuu vya pili vya Dunia.  Mwaka mmoja baadaye timu sita zilishiriki michezo huko Stoke Mandeville -- kukiwa na mashindano ya netiboli, mchezo uliotangulia mchezo wa kikapu -- wakati michezo ikitumiwa kama sehemu ya matibabu ya wagonjwa kama ilivyopengekezwa na Guttmann.  Mwaka 1956, ''taarifa ya dhamira''ilizinduliwa kwa ajili ya Michezo hii ambayo wakati huu ilikuwa ni ya Kimataifa kwa mujibu wa wavuti ya kumbukumbu za Mandeville inayodhaminiwa na mamlaka ya wilaya hiyo.  Washiriki kutoka Niger London 2012  Taarifa hiyo ilisema 'dhamira ya michezo ya Stoke Mandeville ni kuwaunganisha wanaume kwa wanawake waliopooza viungo kutoka sehemu zote za Dunia katika vuguvugu hili la michezo ya Kimataifa, pamoja na moyo wa wanamichezo hii leo kuwapa matumaini na kuwa kivutio kwa maelfu ya walemavu.  Miaka minne baada ya hapo, wakivutiwa na muongozo wa Guttman, mashindano ya kwanza ya Walemavu yakafanyika mjini Roma sambamba na Olimpiki.  Miaka hamsini baada ya michezo ya kwanza kwa walemavu, washiriki 4,280 kutoka mataifa 165 -- ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kujitokeza kushiriki -- wamerejea Uingereza kushiriki mashindano ambayo hivi sasa yanashirikisha watu waliozaliwa na hali hio kutokana na sababu mbalimbali labda ajali au kusababishwa na maradhi.  Tangu michezo hii ianzishwe huko Stoke Mandeville, jina linalotumiwa na kibonzo mleta bahati mwenye jicho moja au ''Mascot'' wa michezo, kwa hakika Michezo hii imepiga hatua kubwa.  Lengo la mashindano haya siyo kuwapima uwezo, bali kuwawezesha kufurahia uwezo wao moyo wa michezo hii umebaki pale pale.



No comments:

Post a Comment