Bao la Cristiano Ronaldo katika
dakika ya mwisho ya mchezo liliiwezesha klabu ya Real Madrid kuishinda
Manchester City magoli 3-2 walipowakaribisha katika uwanja wao wa
Bernabeu nchini Uhispania, mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kipa Joe Hart kwa muda mrefu aliiwezesha Man
City kuendelea vyema pasipo kufungana mabao katika mechi ya Jumanne
usiku, hadi Edin Dzeko alipowashangaza wenyeji kwa kupata bao katika
kipindi cha pili.Marcelo alisawazisha, kupitia mpira ambao ulimgusa mchezaji wa City kabla ya kubadilisha mwendo, lakini City wakafanikiwa kuendelea tena kuongoza baada ya mkwaju wa free-kick kutoka kwa Aleksandar Kolarov, wakati mpira moja kwa moja ulielekea hadi wavuni.
Kisha Karim Benzema aliweza kusawazisha, kabla ya Ronaldo kuandikisha bao la tatu na la ushindi katika mechi hiyo, na matokeo yakawa 3-2.
Kati ya mechi nyingine za klabu bingwa barani Ulaya ilikuwa ni pamoja na mchezo wa Arsenal, ambayo ilianza kampeni yake ya 15 ya mashindano hayo kwa kuwashinda wageni katika michuano hiyo, Montpellier ya Ufaransa.
Timu ya Arsene Wenger ililemewa ugenini baada ya dakika tisa, wakati nahodha Thomas Vermaelen aliposababisha penalti,ambayo ilifungwa na Belhanda, lakini kutokana na magoli mawili ya Arsenal kupatikana kwa haraka katika kipindi cha kwanza, kutoka kwa Lukas Podolski na Gervinho, hali ya mchezo ilibadilika, na Arsenal ikapata ushindi wa magoli 2-1.
Ushindi huo unamaanisha Arsenal na Schalke ya Ujerumani ndio vilabu ambavyo vinaongoza katika kundi B.
No comments:
Post a Comment