BALOZI wa Palestina hapa nchini, Dk Nasri Abujaish amesema
ushindi iliyoupata nchi yake baada ya kupigiwa kura na hatimaye
kuipandisha hadhi ni ushindi wa dunia nzima katika kupigania haki za
binadamu, uhuru na amani.
Dk Abujaish aliyasema hayo juzi alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ubalozi huo, zilizopo
Upanga ,jijini Dar es Salaam.
“Huu ni ushindi wa dunia nzima kwa ajili ya haki
za binadamu, uhuru, utaifa na amani. Kwa hili ulimwengu useme sasa
‘yatosha kwa utawala na ukandamizaji’,” alisema Dk Abujaish.
Hivi karibuni Baraza la Umoja wa Mataifa
lilipitisha kwa kauli moja kwa wingi wa kura, kupandisha hadhi ya eneo
la Palestina baada ya nchi 138 kuunga mkono hatua ya kuitambua
Palestina kuwa nchi ambayo si mwanachama wa Umoja wa Mataifa lakini
itaruhusiwa kushiriki katika shughuli za umoja huo.
Hata hivyo mataifa tisa yakijumuisha Israel na
Marekani yalipiga kura ya kupinga mpango huo, huku mataifa 41 yakisusia
shughuli hiyo.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa, sasa inaiwezesha Palestina kuwa na ushirika katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kama vile Mahakama ya ICC.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa, sasa inaiwezesha Palestina kuwa na ushirika katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kama vile Mahakama ya ICC.
Alisema baada ya hatua hiyo, Palestina itakuwa na
uwezo wa kuzitumia mamlaka za Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa
ya uhalifu wa kivita na inaweza kuishtaki Israel kutokana na vitendo
vyake vilivyo kinyume cha haki za binadamu.
Alisema chini ya hatua hiyo, wafungwa wa kisiasa watakuwa wakichukuliwa kama wafungwa wa vita chini ya Azimio la nne la Geneva.
Alisema chini ya hatua hiyo, wafungwa wa kisiasa watakuwa wakichukuliwa kama wafungwa wa vita chini ya Azimio la nne la Geneva.
“Kutokana na ushindi huo, uvamizi wa Israel
unakuwa umekataliwa na Taifa la Palestina limeshinda. Tunatumai kuwa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakubali ombi la Palestina
lililowasilishwa mwaka 2011 la kuipa uanachama wa moja kwa moja na
kufikia mwafaka wa mipaka ya nchi mbili ulioanza tangu mwaka 1967,”
alisema.
Alisema ushindi huo pia utawawezesha kutafuta suluhisho kati yake na Israel kuhusu matamko yaliyokiuka sheria, Mji wa Jerusalem, mipaka, wakimbizi maji na rasilimali nyinginezo.
Alisema ushindi huo pia utawawezesha kutafuta suluhisho kati yake na Israel kuhusu matamko yaliyokiuka sheria, Mji wa Jerusalem, mipaka, wakimbizi maji na rasilimali nyinginezo.
“Nazishukuru nchi 138 zilizoipigia kura Palestina,
zinatoka Afrika, Asia, Marekani Kusini na sehemu ya Ulaya. Kwa kipekee
kabisa tunaishukuru Tanzania kwa kusimama upande wetu. Kwa mara nyingine
imeonyesha mshikamano wa kihistoria uliokuwepo,” alisema.
Kuhusu mataifa yaliyopiunga mpango huo, Dk Abujaish alisema yanakwenda kinyume na kanuni za haki za binadamu zinazodai kuzipigania.
Kuhusu mataifa yaliyopiunga mpango huo, Dk Abujaish alisema yanakwenda kinyume na kanuni za haki za binadamu zinazodai kuzipigania.
Kwa muda mrefu sasa, Palestina imekuwa
ikishinikiza kutambuliwa kuwa ni taifa huru, lakini imekuwa ikipata
vipingamizi kutoka Marekani na washirika wake ikiwamo Israeli.
Hata hivyo kiongozi wa palestina Mahamood Abbas, ameapa kuendelea na jiotihada za kuushinikiza Umoja wa Mataifa na mataifa mengine duniani, ili yakubali kuitambua Palestina.
Hata hivyo kiongozi wa palestina Mahamood Abbas, ameapa kuendelea na jiotihada za kuushinikiza Umoja wa Mataifa na mataifa mengine duniani, ili yakubali kuitambua Palestina.
Nchi hiyo imekuwa ikipinga vikali utawala wa
mabavu wa Israel ambayo imekuwa ikikalia baadhi ya maeneo yake, jambo
linalosababisha kukua kwa mgogoro wa mara kwa mara.
Hata hivyo mataifa mbalimbali duniani yamekuwa yakihimiza amani.
Hata hivyo mataifa mbalimbali duniani yamekuwa yakihimiza amani.
No comments:
Post a Comment