TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, jana
ilitinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kuifumua
Somalia mabao 7-0, huku mshambuliaji wake Mrisho Ngasa akicheka na
nyavu mara tano.
Kwa ushindi huo wa kishindo, Kili Stars imetinga robo fainali ya michuano hiyo ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili na kufungwa moja dhidi ya Burundi katika hatua ya makundi kwenye kundi la B.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Lugogo badala ya Namboole kutokana na ubovu, mabao mawili ya Kili Stars yalifungwa na John Bocco ‘Adebayor’, hivyo vijana wa Kocha Kim Poulsen kutinga robo fainali huku Somalia ikirejea nyumbani bila pointi.
Ngasa, nyota wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, alikuwa wa kwanza kuipatia bao Kilimanjaro Stars katika dakika ya kwanza, kabla ya kurudi tena nyavuni dakika ya 23 kuipa Kili Stars bao la pili.
Dakika tatu baadaye, Bocco aliifungia Kili Stars bao la tatu, kabla ya kuongeza la nne dakika ya 42.
Ngasa alikihitimisha kipindi cha kwanza kwa bao la dakika ya 45, katika mechi ambayo ilionekana kama ya upande mmoja chini ya mwamuzi Ronnie Kalema wa Uganda.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kuonesha uchu wa mabao zaidi, ambapo Ngasa alifunga mara mbili katika dakika za 74 na 75 za mtanange huo wa kundi C la michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Huo ni ushindi wa pili wa kikosi cha Kili Stars chini ya Poulsen, ambacho kilifungua hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan, kabla ya kuangukia pua kwa kufungwa bao 1-0 ilipoumana na Burundi, mechi zote zikipigwa kwenye dimba la Namboole.
Wakati Stars ikijikatia tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano hii, Somalia imejikuta ikimaliza kwa aibu zaidi, baada ya kuondoka mashindanoni ikiruhusu kufungwa jumla ya mabao 13 yenyewe ikifunga moja katika mechi zake tatu za kundi B.
Somalia ilifungua kwa kichapo cha mabao 5-1 mbele ya Burundi, kisha ikadonyolewa bao 1-0 ilipocheza na Sudan, kabla ya gharika hii iliyoshushiwa na Kili Stars jana.
Mechi ya mwisho kundi hilo itapigwa leo, ambapo Burundi itakwaana na Sudan kwenye Uwanja wa Wankulukulu.
Katika mfululizo wa michuano hiyo, timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ ambayo imeshafuzu kwa robo fainali, leo inashuka kwenye Uwanja wa Wankulukulu, kupepetana na timu mwalikwa, Malawi, katika pambano linalotarajiwa kuwa kali.

No comments:
Post a Comment