Chama cha
upinzani nchini Ghana kimepinga matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa urais
ambayo yalimpa ushindi rais John Mahama.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa bwana Mahama
alishinda kwa asilimia hamsini na saba ya kura na kuondoa uwezekano wa
kufanyika duru ya pili ya uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake Nana
Akufo-Addo aliyepata asilimia 47 ya kura.Ghana imejipa sifa ya kuwa nchi yenye demokrasia thabiti barani Afrika na moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika.
Kwa upande wake rais Mahama aliwataka watu kuheshimiana kufuatia matangazo ya kura ambayo yalimpa ushindi.
Hapakuwa na ripoti zozote za ghasia Jumatatu asubuhi baada ya matangazo ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kutangazwa siku ya Jumapili.
Furaha na nderemo zilijaa punde baada ya matangazo, huku mamia ya watu wakijitokeza kuonyesha furaha yao kwa ushindi wa rais Mahama.
this thing is killing african
ReplyDelete