Kama unakumbuka kwenye consert
ya Summer Jam mwaka huu ambayo huandaliwa na kituo maarufu cha radio cha
Marekani HOT 97 kuna mtangazaji mmoja aitwae Rosenberg alipokua kwenye
stage ya hiyo Fiesta yao a.k.a Summer Jam alimchana rapper Nicki Minaj
kwa kusema aliacha kufanya hiphop na kuanza kufanya muziki wa pop kitu
ambacho kitamuharibia mwelekeo wake wa muziki.
Sasa hivi Nicki Minaj ametoa album ya Pink Friday the re-up, hii ni ile ile album kama ya mwanzo ila kwenye hii mpya kaongeza track 6 ambazo nyingi ni hiphop zaidi ya pop.
Kwenye wiki ya kwanza imeuza
kopi elfu 36 tu kitu ambacho ni kibaya sana kwa staa kama yeye, baada ya
Msanii mkubwa kama Nicki kuporomoka hivyo kwenye mauzo, watangazaji
wengine wa Hot 97 wakaongea kwenye show kwamba Rosenberg alipomchana
Nicki ni kama alitabiri na alikua sahihi
Baada ya hao watangazaji
kuongea hivyo, mkuu wa vipindi wa Hot 97 anasema alipokea simu kutoka
kwa Nicki Minaj ambae alizungumza maneno yote makali ambayo wanawake
huwa wanatumia kuwatukana wanaume, akamuita rafiki wa uongo na tapeli na
kusema ameambiwa na watu huyu mshkaji sio mtu mzuri.
Ebro ambae ndio mkuu wa vipindi
akamjibu Nicki akisema “mimi nilikua najaribu kukujenga maana najua
hiphop ina ushindani na usipobaki kwenye ramani ya hiphop
usipozungumziwa kwenye hiphop utasahaulika, nakupenda sana Nicki na hata
kikiharibika au ukianguka nitakuinua na kukurekebisha ulipokosea, ndio
hapo Nicki Minaj akanitamkia kwamba kwanza msicheze tena nyimbo zangu
kwenye radio yenu”
Pamoja na hayo maneno makali ya
Nicki Minaj mkuu huyo wa vipindi wa Hot 97 New York amesema radio yao
itaendelea kucheza muziki wa Nicki Minaj kwa sababu anampenda.
CHANZO MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment