Thursday, December 6, 2012

Waandamanaji waizingira ikulu Misri,ni muendelezo wakupinga mamlaka Rais aliyojiongezea

Makabiliano yamezuka kati ya wafuasi wa Rais wa Misri Mohammed Morsi na wapinzani wake nje ya ikulu ya rais mjini Cairo.

Wafuasi wa rais huyo wameharibu mahema yaliyowekwa nje ya ikulu hiyo na wapinzani wa Morsi walioanza kukesha nje ya ikulu hiyo Jumanne kupinga mamlaka aliyojilimbikizia.
Pia wanapinga rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura ya maoni tarehe 15 mwezi Disemba
Makamu wa rais Mahmoud Mekky,amesema kuwa mabadiliko yaliyofanyiwa katiba hiyo yanaweza kukubalika na upinzani.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton amesema mazungumzo yanahitajika haraka kuhusu katiba hiyo.
Maelfu ya wapinzani wa rais wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo.
Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo.
Maelfu wameizingira ikulu wakimpinga rais kwa kujilimbikizia mamlaka
Siku ya Jumanne , maelfu ya waandamanaji walivamia ikulu wakipinga rasimu ya katiba iliyozua utata mkubwa pamoja na kupinga sheria inayomlimbikizia mamlaka makuu Rais Morsi.
Wakati mmoja polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao walikuwa wamevuka ukuta wa seng'enge. Vikosi vya usalama vilitoa taarifa vikisema kuwa rais Morsi ameondoka katika ikulu hiyo na ameomba utulivu.
Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais kujilimbikizia madaraka mapya na kusababisha kuundwa kwa rasimu ya Katiba.
chanzo-bbc.com

No comments:

Post a Comment