Kikao hicho kilichoanza jana katika Hotel ya Blue
Pearl, kinatarajia kuendelea leo na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel
Natse, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso, Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Karatu, Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini, Jubiless Mnyenye
watahojiwa.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza jana
kuwa wabunge pamoja na viongozi wa Chadema wa jimbo hilo hawaelewani na
ndiyo chanzo cha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo, ukiwamo wa Maji
Karatu Vijijini (Kaviwatu).
Kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichokaa
Septemba 9 mwaka huu, kiliunda Tume ndogo ya kuchunguza suala hilo
ambayo ilipendekeza baadhi ya madiwani kuchukuliwa hatua.
Katika kikao cha jana, ajenda kuu zilizokuwa zikijadiliwa ni taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha dharura cha Septemba 9, mwaka huu.
Katika kikao cha jana, ajenda kuu zilizokuwa zikijadiliwa ni taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha dharura cha Septemba 9, mwaka huu.
Katika kikao hicho mbali ya kuagiza chama
kimwandikie barua rasmi Rais Jakaya Kikwete ili asimamie utekelezaji wa
baadhi ya masuala yaliyoko kwenye mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya
Nchi, pia kiliazimia masuala kadhaa.
Mambo hayo ni pamoja na kuwataka Waziri wa Mambo
ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta
Jenerali, Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna
Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile,
wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.
Pia kiliazimia kwamba Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa
Morogoro na askari waliosababisha mauaji ya raia wasio na hatia Morogoro
na Iringa wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Mbali na kupokea taarifa hiyo kikao hicho pia
kilijadili hali ya kisiasa nchini, mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya
nchi na Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).
Bavicha wakana
Bavicha wakana
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana Chadema (Bavicha), Mkoa wa Mwanza, Liberatus Mulebele amesema
hakuna vijana wa chama hicho ambao wamemkataa Katibu Mkuu, Dk Willibrod
Slaa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana,
Mulebele amesema yeye ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu
Bavicha kwa Mkoa wa Mwanza na kwamba hakuna mtu mwingine.
“Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza
hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya
Chadema na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwamo
Katibu Mkuu, Dk Slaa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kiongozi huyo amesema vijana wa Chadema Mkoa wa Mwanza wako pamoja akisema waliotoa taarifa za kumtuhumu Dk Slaa si wenzao.
No comments:
Post a Comment