BARAZA la madaktari Tanganyika limewasimamisha kwa muda
madaktari 30, kutoa onyo kwa madakari 289 na kuwafutia mashtaka
madaktari 49 baada ya kupitia malamamiko ya Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kufuatia mgomo wa madaktari uliotokea Juni 23 hadi 28 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara
hiyo, Nsachris Mwamwaja imeeleza kuwa Baraza lilipitia malalamiko yote
na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki
katika mgomo huo.
Alisema mashtaka yaliyoahirishwa kutokana na
wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria ni madaktari wanne na mashtaka
yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza ni
madaktari 22.
“Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa
mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao
walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari,”aliseleza Mwamaja
na kuongeza
“Wizara pia imeridhia kuwapa madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.”
“Wizara pia imeridhia kuwapa madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.”
Hata hivyo alisema fursa hiyo haitawahusu
madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari,
hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
Alisema kwa taarifa hiyo madaktari wote
waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa
kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua
kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa
usajili na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo.
Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu ili kupewa
barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.
barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.
No comments:
Post a Comment