Thursday, December 6, 2012
HIZI NDIO SENTENSI KUTOKA SIMBA KUHUSU AZAM FC KUMUUZA NGASA SUDAN.
Jana club ya Simba ilitangaza kumuuza mchezaji wake Mrisho Ngassa anaecheza Simba kwa mkopo kwa El-mereikh ya Sudan ambapo taarifa iliyotolewa na Azam ilisema mchezaji huyo ameuzwa kwa dola za kimarekani zaidi ya elfu hamsini na sasa anasubiri kumaliza michuano ya Cecafa kisha aende Sudan kucheki mazingira.
Baada ya hiyo taarifa kutoka Uongozi wa Simba umetoa tamko kupitia mwenyekiti Ismail Aden Rage kwenye Sports Extra ya Clouds fm na kusema kilichofanywa na Azam Fc ni kitendo cha kihuni.
Namkariri akisema “jambo hili limetusikitisha sana, halikufata taratibu kanuni na sheria za mpira wa miguu kwa sababu mchezaji Ngassa tulitangaziwa anauzwa na kwamba club itakayotoa pesa nyingi ndio itamchukua hivyo sisi tukatoa milioni 25 na tukasaini mkataba kwamba kwa hizo milioni 25 tutamtumia kwa mwaka mmoja baada ya hapo hatutakua na haki nae labda kama tutakubaliana tena”
Kwenye sentensi nyingine Rage amesema “vilevile katika huo mwaka mmoja tulikubaliana tutamlipa mshahara na marupurupu, sasa jambo la kusikitisha hawa ndugu zangu wameongea kwamba wametupa kwa mkopo, ukishalipa pesa lile neno la mkopo halipo tena yule ni mchezaji wetu halali kabisa na wala hawana mamlaka yoyote ya kumuuza bila idhini yetu, swala hili tutalipigania mpaka dakika ya mwisho na tumewasiliana na TFF wakatuhakikishia haiwezekani hata kidogo Azam wakafanya hivyo bila kufata utaratibu”
Ameamplfy zaidi kwamba El Mereikh walimfata Ngassa kabla ya kwenda Azam akawaambia yeye hawezi kuzungumza chochote hivyo wakaenda kwa uongozi wa Simba ambao uliitaka timu hiyo ya Sudan kuweka mezani dola laki mbili na nusu na sio laki moja na nusu waliyokua nayo.
Alipoulizwa kama kwenye makubaliano ya mkataba na Azam kuna neno mkopo Aden Rage kwa ufupi jibu alilotoa linamaanisha hakuna neno mkopo, anasema Ngassa hakutolewa kwa mkopo ni kwamba alinunuliwa.
chanzo-millardayo.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment