Kama wewe ni shabiki wa soka la
bongo na umekua ukilifatilia, hii ni nafasi yako kusikia aliyoyasema
mchezaji Uhuru Selemani aliyehamia Azam Fc akitokea Simba Sc.
Kwenye exclusive interview na
AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, Amesema kwenye maisha yake ya soka kuna mambo
mawili tu ambayo yamewahi kumuumiza sana, moja ni kifo cha Patrick
Mafisango aliekua akicheza nae Simba na jingine ni kuwekwa benchi kwa
msimu mzima Simba.
Kuhusu sababu za yeye kuwekwa
benchi kwa msimu mzima namkariri akisema “sitaki kuficha, mi naamini
kuna kiongozi mmoja ndani ya Simba ambae alikua hataki mafanikio yang
lakini sielewi kwa nini namjua kabisa ila siwezi kutaja jina lake”
“Nafikiri huyo mtu alikua
karibu sana na mwalimu na alikua na nafasi ya kuongea sana na mwalimu
kwa hiyo ndio alikua anapanga mimi nisitumike kwenye timu, sijui ni kwa
sababu gani na sijawahi kukorofishana nae” – Uhuru
Kwenye sentensi nyingine Uhuru
amesema kuhusu kukaa kwake benchi aliwahi kumuuliza mwalimu lakini
hakumjibu chochote zaidi ya kumwambia kwamba yeye ni mchezaji bora
anatakiwa kuendelea kufanya mazoezi manake ni mchezaji mzuri ambae
anaweza kufanya kitu chochote.
Namkariri tena akisema “mwalimu
alikua halioni hilo, viongozi wa juu wa timu waliliona pia lakini
walinyamaza kama rais wa timu ananijua nina mchango gani kwenye timu
lakini hakuwahi kuuliza hata siku moja kwa nini Uhuru hachezi”
Kwa kumalizia Uhuru amesema
“Kukaa benchi bila kupewa jezi imeniuma sana, nataka watu wajue hiyo
imeniuma sana na sikutegemea kama Simba wanaweza kunifanyia kitu kama
hicho kwa sababu nimeifanyia Simba mambo makubwa sana, nimeingia Simba
nimeipa taji la ubingwa mara mbili, makombe mbalimbali na ngao za
hisani.. ni kwa muda mfupi ambao nimekuwepo Simba japokua kuna watu
ambao nashirikiana nao lakini kwa upande wangu naamini nimetoa mchango
mkubwa”
CHANZO-MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment