RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja
Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu.
Kwa
mujibu ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inaeleza kuwa maofisa wakuu
waliopandishwa cheo ni Meja Jenerali, Sylvester Chacha Ryoba ambaye ni
Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Luteni
Jenerali.
Mwingine ni Meja Jenerali, Charles Lawrance Makakala ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Rais Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewapongeza wakuu hao.
Wakati
huohuo, Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kufanya ziara ya siku moja
mjini Rufiji, licha ya mambo mengine atahutubia mkutano wa hadhara
mjini Ikwiriri.
Akizungumza jana kwenye Baraza la Madiwani, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard
Rwegasira alisema Rais Kikwete atapokelewa mpakani mwa wilaya ya Kilwa
na Rufiji, eneo la Malendego.
Rwegasira alisema wananchi wa
Rufiji wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo
atakapoingia wilayani hapa ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu
kumalizika kwa Uchaguzi Mwaka 2010.
Hata hivyo, Rwegasira aliwataka madiwani kuwajulisha wananchi kushiriki kumpokea.
No comments:
Post a Comment