RUFAA ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA),
jana iliunguruma katika Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, huku Wakili
anayemtetea Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Vitalis Timon, akidai kwamba,
Lema hakustahili kuvuliwa ubunge kwa kuwa alishinda kihalali.
Pamoja na hayo, Timon alidai mahakamani hapo, kwamba wanachama watatu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopinga ubunge wa Lema hawana haki ya
kufanya hivyo na kwamba matusi hayawezi kumvua ubunge.
Kwa
mujibu wa Timon, matusi hayawezi kumvua ubunge Lema, kwani wabunge
wenyewe walitunga sheria namba nane ya mwaka 1995 ambayo inaruhusu
matusi baada ya kuona awali walikuwa wakibanwa na mahakama.
Wakili Timon alidai hayo jana, katika Mahakama ya Rufaa, mbele ya jopo
la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Benard Luanda,
wanaosikiliza rufaa hiyo iliyokatwa na Lema, akipinga uamuzi wa Mahakama
Kuu, Kanda ya Arusha wa kumvua ubunge.
Lema alivuliwa ubunge
Aprili 5 mwaka 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu
wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel.
“Mpiga
kura hawezi kupinga matokeo ya uchaguzi wakati yanayotokea katika
kampeni hayamhusu, mpiga kura si sehemu ya Kamati ya Maadili na hana
haki katika kampeni.
“Ushahidi uliotolewa ni matusi dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM ambaye ni Batilda Buriani.
“Ubaguzi wa kidini, kijinsia na makazi, mambo hayo yana athari gani kwa
wanachama wa CCM waliofungua kesi ya uchaguzi namba 13/2010 Arusha?
No comments:
Post a Comment