Bunge la taifa la Libya
limeagiza kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo na mataifa ya Sudan, Niger,
Chad na Algeria na kutangaza mikoa saba Kusini mwa nchi hiyo kusimamiwa
na jeshi chini ya sheria ya hali ya hatari.
Msemaji wa bunge hilo Omar Humidan amesema kuwa
hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama na inalenga kuzuia
wahamiaji haramu na bidhaa kuingia nchini humo kupitia mipaka ya Libya
na mataifa hayo.Maeneo ya Kusini mwa Libya yameshuhudia visa vingi vya ukiukwaji wa sheria tangu kuondolewa kwa rais Muammar Gadaffi mwaka uliopita.
Waasi watoroka Kaskazini mwa Mali
Mbunge mmoja, Suad Ganur,amesema hali katika maeneo hayo imeendelea kuwa mbaya katika siku za hivi karibuni kutokana na hofu ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu Kaskazini mwa Mali.Afisa huyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, visa vya ghasia na machafuko na ulanguzi wa mihadarati vimeendelea.
Amesema makundi mengi ya watu waliojihami yameongeza sana katika eneo hilo na yamekuwa yakihudumu bila kujali sheria zilizopo.
Tangazo hilo limetolewa baada ya muungano wa Ulaya kupendekeza utasaidia katika harakati za kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Libya ili kulinda maeneo ya mipaka yake ya Kusini ili kuzuia wanamgambo hao kuigizasilaha ndani ya nchi hiyo.
Azimio hilo lililopitishwa na bunge linasema maeneo ya Kusini ya Ghadames, Ghat, Obari, Al-Shati, Sebha, Murzuq na Kufra sasa, yatakuwa chini ya uongozi na uthibiti wa jeshi la taifa chini ya sheria hiyo ya hali ya hatari.
No comments:
Post a Comment