Kgalema Motlanthe (Kushoto) na rais Jacob Zuma
Msemaji wa makamu wa rais wa
Afrika kusini Kgalema Motlanthe amesema amekubali uteuzi wake kugombea
uongozi wa chama tawala nchini humo cha African National Congress.
Msemaji huyo Thabo Masebe amesema bwana Montlanthe atagombea kiti cha urais cha ANC, makamu wa rais na nyadhifa nyingine .Atawania kiti hicho wiki ijayo ambapo atakabiliana na rais wa sasa wa Afrika kusini Jacob Zuma katika mkutano wa chama utakaofanyika Bloemfontein.
Waandishi wa habari wanasema yeyote atakayekuwa kiongozi wa ANC atakuwa na nafasi nzuri ya kuwa rais ajae katika baada ya uchaguzi wa mwaka 2014
No comments:
Post a Comment