Hatimae club ya Simba
imethibitisha kuvunja mkataba na kocha wake Mserbia Milovan Cicovic
ambapo sasa wanatarajia kumtambulisha kocha mpya kutoka Ufaransa.
Namkariri afisa habari wa Simba
Ezekiel Kamwaga akisema “huyu kocha ana uzoefu mkubwa sana zaidi ya
ukocha wa kufundisha timu kubwa alianzia maisha kwenye Academy, amepitia
Academy ya ufaransa ambayo ni maarufu sana na ndiyo iliyotoa kina
Thiery Henry wakati huo, mbali na timu kubwa atatutengenezea mfumo mzuri
wa kutengeneza timu yetu ya vijana, sasa hivi Tanzania tunashindana na
timu mbili za mamilionea”
Kwenye line nyingine Kamwaga
amesema “atasaidia kukuza viwango vya wachezaji wetu, kama atakua na
Simba nzuri manake na timu ya taifa pia itafaidika kwa sababu Simba ndio
tegemeo la timu ya taifa ya Tanzania”
Kuhusu ishu nzito ya kumuuza
mchezaji Mrisho Ngassa kwenda kucheza Sudan Kamwaga amesema “sisi
tumeshakubaliana na Azam kwamba Ngassa akiuzwa basi tutagawana nusu kwa
nusu lakini cha msingi Ngassa hawezi kuchezea timu nyingine hapa
Tanzania ambayo siyo Simba kwa sababu tuna mkataba nae unaoisha May,
Ngassa bado ni mchezaji wetu na tunataraji kwamba mwishoni mwa wiki hii
atajiunga kwenye mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa sasa na ligi
kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa”
“Wanasema yeye
aliongea na hiyo timu ya Sudan na kukubaliana kulipwa dola za
kimarekani elfu 70 kwa hiyo Kama atataka kwenda Sudan atakwenda, kama
hatokwenda sisi tutamtumia lakini hatuwezi kumpandisha ndege au
kumlazimisha, kama atakwenda tutampa ushirikiano kwa asilimia 100 na
kama hatotaka kwenda pia tutampa ushirikiano kwa asilimia 100″ – Kamwaga
Kwenye sentensi ya mwisho
Kamwaga amesema mlinda mlango namba moja Afrika Mashariki anaetokea
Uganda ameshaingia Dar es salaam tayari na anafanyiwa vipimo vya Afya
kwenye hospitali moja na kama atafaulu basi atasajiliwa na Simba.
chanzo-millardayo.com
No comments:
Post a Comment