Wapinzani hao wa kisiasa, wanatarajiwa kupambana
kwa hoja za kisheria, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Ng’humbi ya
kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyomthibitisha
Mnyika kuwa mbunge halali wa Ubungo.
Mnyika, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), alitangazwa na Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Ubungo,
kuwa mbunge wa jimbo hilo, baada ya kupata kura 66,742 huku Ng’umbi
akipata kura 50544.
Hata hivyo Ng’humbi kupitia Wakili wake, Issa
Maige alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi huo wa Mnyika, huku
akiiomba mahakama ibatilishe matokeo na kuamuru uchaguzi huo urudiwe.
Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 107 ya
mwaka 2010 na wakati wa ushahidi wake mahakamani, Ngh’umbi alidai kwamba
kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na kanuni za sheria wakati wa
kampeni, ujumlishaji na utangazaji matokeo.
Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake, ilitupilia mbali madai ya Ng’humbi na badala yake ikamthibitisha Mnyika kuwa mbunge.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa Mei 24, 2012, Jaji
Upendo Msuya alisema upande wa madai ulishindwa kuyathibitisha madai
yake pasi na shaka, huku akidai kuwa ushahidi wa Ng’humbi ulikuwa ni
maneno ya kusikia tu ambayo hakuyashuhudia.
Hata hivyo, Ng’humbi hakukubaliana na hukumu hiyo
na kuamua kukata rufaa akiiomba mahakama ya rufani itengue hukumu hiyo
ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Rufaa hiyo imepangwa kuanza
kusikilizwa leo na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani; Salum
Massati, Katherine Oriyo na Nathalia Kimaro.
Ng’humbi katika rufaa yake hiyo aliyoifungua Oktoba 25, 2012,
Kupitia kwa wakili wake, Maige, ameorodhesha hoja kumi za kupinga hukumu hiyo, akidokeza kile anachokiona kuwa ni udhaifu katika hukumu.
Pamoja na mambo mengine, Ng’humbi anadai kuwa Jaji Msuya alikosea katika kutafsiri sheria na kupima ushahidi wa pande zote.
Kupitia kwa wakili wake, Maige, ameorodhesha hoja kumi za kupinga hukumu hiyo, akidokeza kile anachokiona kuwa ni udhaifu katika hukumu.
Pamoja na mambo mengine, Ng’humbi anadai kuwa Jaji Msuya alikosea katika kutafsiri sheria na kupima ushahidi wa pande zote.
Baadhi ya hoja zake katika rufaa hiyo, Ng’humbi
anadai kuwa jaji alikosea kusema kuwa makosa yaliyobainika katika
ujumlishaji na kuhesabu kura na kusababisha kuwapo kwa kura 14,854,
zisizohesabiwa hayakuathiri matokeo ya uchaguzi.
Anadai kuwa alithibitsha makosa katika mchakato wa
uchaguzi yaliyosababisha kuwapo kwa kura 14, 854 zisizohesabiwa, hivyo
jaji alikose kwa kutokuhamishia kwa mdaiwa, jukumu la kuelezea sababu
za kuwapo kwa dosari hizo.
“Jaji alijipotosha kumshutumu mrufani kwa
kutokubainisha kuwa makosa ya msingi yaliyobainika katika kujumlisha na
kuhesabu kura yalikuwa ni ya nia mbaya,” inasisitiza hati hiyo ya rufaa
na kuongeza:
No comments:
Post a Comment