Wednesday, December 19, 2012

Kagame aonywa dhidi ya kuwasaidia waasi



Rais Barrack Obama wa Marekani ametoa wito kwa rais wa Rwanda Paul Kagame, kusitisha msaada anaotoa kwa makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Barack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama
Kwa mujibu wa ikulu ya White House, rais Obama alifanya mazungumzo ya simu ya Rais Paul Kagame siku ya jumanne, ambapo aliafiki tangazo lake la kujitolea katika harakati za kupatikana kwa amani katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waasi wa M-23 wapo katika eneo la mashariki mwa Congo licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kutunza amani wa umoja wa mataifa katika eneo hilo.
Ripoti ya hivi majuzi iliyochapishwa na Umoja wa Mataifa iliishutumu serikali ya Rwanda kwa kutoa msaada kwa waasi hao wa Congo, madai ambayo serikali ya Rwanda Imekanusha vikali.

No comments:

Post a Comment