Papa Benedict anafungua akaunti katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa kanisa katoliki.
Taarifa kuhusu akaunti hiyo itatolewa baadaye
hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini duru kutoka Vatican
zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo.Kanisa hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.
Wakatoliki kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.
Papa Benedict anataka kuitumia akaunti hiyo kuwasiliana na wakatoliki kote duniani.
chanzo-bbc
No comments:
Post a Comment