Akizungumza baada ya kesi kufutwa Mnyika amesema mwanzoni alitarajia mpinzani wake asingeweza kuendelea na kesi hiyo kutokana na kutokuwa na vielelezo vya msingi ambavyo visingeweza kumsaidia kushinda rufani hiyo.
May 24 2012 John Mnyika alishinda kesi ya uchaguzi 2010 baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam kutupilia mbali mashtaka yote matano yaliyokua yakimkabili ikiwa ni pamoja na kutumia laptop wakati wa kuhesabu kura, idadi kubwa ya wanachama wa Chadema kuingia kwenye chumba cha kuhesabia kura, kuwepo kwa kura hewa 16,000 pamoja na kukosewa kwa karatasi za kujumlisha kura.
Namkariri akiongea baada ya kushinda kesi “kesi hii imetuchukulia miaka miwili pamoja na kuwa tulikua tukifanya kazi lakini toka 2010 tumekua tukipotezewa muda Mahakamani kwa sababu ya shauri hili na pamoja na kupotezewa muda huo tumekua tukiwatumikia wananchi jimboni na bungeni, baada ya rufaa hii kuamuliwa decemba 8 nitakua kata ya Manzese ambapo tutaanika hadharani namna ambavyo vigogo wamehusika katika kufuja mali za kiwanda cha urafiki na kusababisha vijana kukosa ajira”
chanzo-millardayo.com
No comments:
Post a Comment