Christopher Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa BBC mwaka wa 2012.
Naodha huyo wa Zambia mwenye miaka 30 amemshinda
Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi
wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika katika historia ya mashindano hayo.Orodha ya washindani hao ilitengazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na wachezaji wengine.
Na idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan Construction.
Katongo aandikisha rekodi mpya
Huku wachezaji wote walioorodheshwa katika kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka mzuri, wanne kati yao walikuwa wameshinda medali mbali mbali, ni Katongo pekee ambaye mafanikio yake yamezingatiwa na mashabiki wa mpira Afrika.Alifunga magoli matatu katika fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon na baadaye kufunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia kunyakuwa kombe hilo.
Zambia iliishindi Ivory Coast kwa 8-7 katika fainali hiyo baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu baada ya muda wa kawaida na muda wa ziada mjini Libreville.
Katongo afufua matumaini ya Zambia kuelekea Brazil
Miezi saba baada ya kuongoza Zambia kushinda kombe hilo, Katongo vile vile amekuwa nyota wa timu yake ya taifa wakati wa michuano ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao,wakati alifunga goli la pekee dhidi ya Uganda.
Bao hilo liliibuka kuwa bao muhimu sana kwa Zambia kwa kuwa ilipoteza mechi iliyofuatia kwa bao moja kwa bila, lakini ikafuzu kwa fainali za mwaka 2013 zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini baada ya kushinda kwa magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.
Mikakati ya kufuzu kwa kombe la Dunia
Na zaidi ya hayo yote, Katongo amechangua pakubwa harakati za kufufua matumaini ya Zambia ya kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2014.Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia ilichuana na Ghana na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyefunga bao la ushindi na hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu.
Ikiwa Christopher Katongo ataendelea na hali aliyo nayo kwa sasa, huenda akaisaidia Zambia kuandikisha matokeo mazuri wakati wa michuano ya kuwania kombe la dunia nchini itakayoandaliwa nchini Brazil miezi kumi na minane ijayo.
No comments:
Post a Comment