Wednesday, December 12, 2012

KUTOKA FOF EXTRAVAGANZAA~~JE UNAIJUA HERUFI YAKO?


Jana tulipokua pale Makumbusho DSM, kwenye FOF(Friends on Friday) Extravaganza kulikua na vitu vingi na tuli enjoy sana kwa wale ambao walikuwepo, kulikua na mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na waimbaji mbalimbali wakiwemo Glorious Celebration, Miriam L mauki, Flora na Emmanuel mbasha na wengine.Bila kusahau nyama choma!
Kuna kitu nataka nikushirikishe wewe mwenzangu ambae hukuwepo, na wewe ambae ulikuwepo nikufikirishee zaidi..



Kuna game moja ambayo ilichezwa, japo haikua mara ya kwanza mimi kuiona ile Game, ila this time niliiona kwa jicho jingine.

Kwa kifupi kulikua na makundi mawili na kila kundi lilikua na watu 6. Wote walipewa karatasi zilizoandikwa herufi moja,so kila upande ulikua na herufi yake. Kiongozi alikua anataja neno nao wanajipanga kutengeneza lile neno liwe kama lilivyotajwa. Ilikua inaenda kwa muda, na kundi litakalowahi kupanga yale maneno ndilo lililokua washindi.

Ilitegemea sana uharaka wa wanakikundi, na ushirikiano wao ili kuweza kujenga neno ambalo wameambiwa, likamilike kwa wakati na lisomeke sahihi.
Ikitokea mmoja kati ya wale wanakikundi amechelewa alikua anawachelewesha wenzake wote. Lakini pia ilihitaji mtu binafsi kwenye kundi ajue kuwa yeye ndio mwenye ile herufi, so kila mtu alitakiwa kujua herufi yake.

Pili kila mtu alitakiwa kuwa makini na neno litakalotajwa ili ajue herufi yake inafit eneo gani. Kama ni mwanzo wa neno au mwisho wa neno.
Mwishoni kundi lililokuwa la kwanza ni lile lililoweza kupanga maneno yake vizuri na kwa wakati, nalo lilishinda na kupewa zawadi ya makofiiii!



 Sasa tunajifunza nini kutoka kwenye hiyo Game?
1. Kila mtu katika kundi alipewa karatasi ambayo ilikua imeandikwa herufi pande zote mbili.
2. Kila mtu alihitaji kujua herufi yake ni ipi.
3. Kila mtu alitakiwa kuwa makini kumsikiliza kiongozi ili kujua ni neno gani linatakiwa na kuweza kujipanga kwnye nafasi yake.
4. Ilihitajika team-work ili kufanikisha zoezi zima.Hata kama mtu mmoja alikua anajua herufi yake na yuko makini kumsikiliza mwalimu lakini kama hakutakua na nguvu kazi ya pamoja bado lengo la kushinda kwa kundi lisingetimia!

Sasa basi, Kila mtu anakitu ambacho Mungu amempa mkononi,amini usamini KILA MTU ana kitu ambacho Mungu amempa.Hicho ndio kipawa au kipaji chako "gift" au "talent". Inawezekana kwa wengine kinaonekana kwa wazi, ni kwa sababu wameamua kuchukua hatua ya kukifanyia kazi.Hata wewe hujachelewa, chukua hatua.

Pili,kama ilivyokua kwenye mchezo ule, kila mtu aliijua herufi yake, ndivyo ambavyo ni jukumu lako wewe kujua kile ulichonacho. Kwa sababu huwezi kusimamia herufi ya mwenzio,lazima iwe ni ya kwako. Ni jukumu lako kuchukua hatua za ziada kujua ni kitu gani ambacho Mungu amekupa.

Tatu, ni kweli kuna Kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako, na unakujua, lakini unahitaji kufuata maelekezo ya namna ya kukitumia. Japo kila mtu alikua na herufi yake na aliijua, babdo alihitaji maelekezo ya kiongozi ili kujua nini cha kufanya kujenga neno waliloambiwa. UnatAka kufikia malengo yako, jifunze kufuata maelekezo..na kama Mkristu kila maelekezo lazima yawe na msingi kwenye Neno la Mungu.

Ilihitajika team work, ili kufanikisha lile zoezi.Biblia inasema Two are better than one..(Mhubiri 4:9), na umoja ni nguvu,ndio maana mwili una viungo vingi, na kila kiungo kina kazi yake.jicho haliwezi kuwa mguu, na kichwa kuwa mkono.Kila mmoja anamhitaji mwenzake ili kuendelea kuishi. Kadhalika vile vitu vyote ambavyo Mungu ameweka ndani yetu tukiviunganisha tunatengeneza kitu kimoja ambacho ndio ilikua kusudi la Mungu kumpa kila mmoja kitu.
Kama ambavyo katika mchezo ule, wote walitegemeana ili kuunda neno moja.

Picha za event zitafuata baadae..

No comments:

Post a Comment