Rio Ferdinand baada ya kujeruhiwa na shabiki mmoja wa Manchester City
Afisa mkuu mtandaji wa Chama cha
wachezaji wa kulipwa wa soka, nchini Uingereza Gordon Taylor, amesema
huenda ikahitajika kujenga ua unaozunguka uwanja ili kuwalinda
wachezaji.
''Mimi nadhani hili ni jambo ambalo tunapaswa kuliangalia zaidi, imependekezwa kuwa ua ujengwe kuuzunguka uwanja hasa katika maeneo yaliyo wazi'' alisema Taylor.
Mashabiki nao wakataa pendekezo hilo
Aliongeza kuwa ujenzi huo unaweza kuwa karibu na maeneo ya goli au karibu na bendera iliyoko katika kila pembe ya uwanja.
Kipa wa Manchester City akimzuia shabiki kumshambulia Rio Ferdinand
Kipa wa Manchester City, Joe Hart, alilazimika kumzuia shabiki mmoja, ambaye alikuwa ameingia uwanjani kutomkaribia Ferdinand, ambaye alikuwa anajaribu kuzuia uso wake kutokana na maumivu.
Lakini mwenyekiti wa chama wa mashambiki wa soka nchini Uingereza, Malcom Clarke, amesema uamuzi wa kujenga ua unaozunguka uwanja sio suluhisho la tatizo hilo.
''Ujenzi wa ua sio jambo ambao tunahisi ni wazo nzuri kwa sasa'' alisema Bwana Clarke.
No comments:
Post a Comment