Thursday, December 6, 2012

CCM Iringa wajitabiria ugumu uchaguzi ujao

CHAMA Cha Mapinduzi mkoani Iringa, kimeshitshwa na taarifa ya Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo kuwa baadhi ya barabara zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa zingetengenezwa kwa kiwango cha lami kama angechaguliwa, hazijatengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.

Katibu wa CCM mkoani humo Emanuel Mteming’ombe, alisema hatua hiyo inakihatarisha chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hasa ikizingatiwa kuwa Rais Kikwete atakakiwa kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho.
“Hii ni hatari kama barabara hizo hazitatengenezwa na kukamilika, jambo hili litatusumbua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa sababu Rais atatakiwa kumnadi mgombea wetu na wananchi watauliza maswali hayo ya ahadi za barabara, ”alisema Mteming’ombe.

Hata hivyo Mteming’ombe alimpongeza Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Paul Lyakurwa kwa jitahadi za kuhakikisha kuwa barabara hizo zinatengenezwa.
Pia aliishauri Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa iliyoketi chini ya mwenyekiti wake Dk Chritine Ishengoma akuihimiza Serikali kutekeleza ahadi hizo.

Akitoa taarifa ya utekeleza wa ahadi za Rais Kikwete katika kikao hicho, Lyakurwa alisema barabara kadhaa ambazo ujenzi wake uliandaliwa mwaka wa fedha wa 2011/13 umesimama kutokana na kutotengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.
Alizitaja barabara hizo kuwa ni ya Rujewa, Madibira Mafinga yenye urefu wa kilometa 151 ambayo alisema upembezi yakiniufu ulishakamilika na kinachosubilrwa ni kupata mkandarasi.Mhandis Lwakurwa alizitaja barabara nyingine kuwa ni ya Ipogolo- Kilolo.

No comments:

Post a Comment