Wednesday, December 12, 2012

Mnyika awataja mafisadi Tanesco

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila hilo la umma.
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Madini na Nishati alisema watu hao ndio wanaoshirikiana kuihujumu Tanesco na kuliingiza taifa katika hasara.
 

Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh alisema uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kuikabidhi ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.

Mnyika aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa walifanya uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na kupendekeza kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza masharti kwa sababu ya mgongano wa maslahi.

Mnyika alipendekeza vigogo hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Aliwataja watumishi wawili ambao walishindwa kutoa taarifa za ukiukaji wa vigezo vya utoaji wa zabuni namba PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya kampuni moja kati ya hizo mblii kupewa zabuni.

Alisema watendaji hao walichangia kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni pamoja na kwamba haikuwa na fedha na kuiwezesha kupewa malipo ya asilimia za ziada kinyume na mkataba.

Akapendekeza watendaji hao kuchuliliwa hatua za kinishamu. nMnyika aliwataja watumishi wengine sita wa Tanesco ambao kwa pamoja walifanya uamuzi uliosababisha kutolewa kwa mkataba namba PA/001/HQ/W/14 wa Machi 11,2010 kwa kampuni hiyo bila kuzingatia uwezo wa kitaalam, kifedha na hivyo kukiuka sheria ya ununuzi wa umma.

Alisema hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuwadhibiti watumishi wa umma wanaoliingiza taifa katika mikataba mibovu.

Mnyika katika taarifa yake hiyo aliwataja wafanyakazi watatu wa Tanesco akieleza kuwa walihusika katika kutoa mapendekezo yaliyowezesha kampuni ya McDonald kupewa mkataba wa zabuni kinyemela.

Mnyika alipendekeza wachukuliwe hatua za kisheria ili kuepusha Tanesco kuingia mikataba kuliongezea shirika mzigo wa gharama na kusababisha ongezeko la bei ya umeme.

No comments:

Post a Comment