Wachezaji 17 kutoka timu ya soka
ya Eritrea na muuguzi wao wanasakwa na maafisa wa usalama nchini Uganda
baada ya kutoweka nchini humo.
Ni wachezaji 12 pekee waliorejea kutoka ziara ya
kununua bidhaa jumapili, na kati ya hawa, watano waliondoka baadaye
wakisema walikuwa wanawatembelea marafiki zao, lakini hawakurejea.Maafisa wa usalama wameanzisha msako wa wachezaji hao waliotoweka walipokuwa mjini Kampala kushiriki mashindano ya mwaka huu ya CECAFA.
" Hatujui ndugu zetu wako wapi, " alisema mkufunzi wa timu Teklit Negash
Tovuti ya chama cha Upinzani nchini Eritrea ilidai kuwa wachezaji hao walikuwa wanataka kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uganda, lakini madai hayo hayajathibitishwa
Naibu rais wa shirikisho la kandanda nchini Uganda (Fufa) anayehusika na masuala ya vijana Patrick Ogwel amethibitisha kuwa wachezaji hao wa Eritrea wametoweka na kusema: " Tutawapata, popote walipojificha."
Na afisaa mkuu wa Fufa Edgar Watson amesema picha za wachezaji hao zitachapishwa magazetini ili kusaidia katika juhudi za kuwasaka.
" Tutawapata kwa kuwa hawako mbali sana, " aliongeza Watson.
Eritrea ilibanduliwa kutoka mashindano hayo ya kikanda ya CECAFA, katika raundi ya makundi baada ya kutoka sare ya bila na Zanzibar, kisha kushindwa 3-2 na Malawi na kuadhibiwa mabao 2-0 na Rwanda katika mechi yao ya mwisho Jumamosi.Sylvia Nakamya, meneja wa Hoteli ya Sky - iliyokuwa makao ya timu hiyo ya Eritrean - alisema wachezaji hao waliondoka Jumapili kuenda kununua vitu kadhaa lakini ni 12 tuu waliorejea.
Nakamya aliongeza: " Baadaye watano kati ya waliorejea, waliondoka wakisema walikuwa wanawatembelea marafiki zao, lakini hawakurejea. "
Baada ya makala ya 2010 ya CECAFA nchini Tanzania, wachezji 13 kutoka timu ya Eritrea pia walitoweka na baadaye kuomba hifadhi ya kisiasa.
Baadhi ya wachezaji hao wamejitokeza Houston, Texas chini ya mpango wa kuwapa makao wakimbizi nchini Marekani.
Wachezaji wa Eritrea waliosafiri kuelekea Uganda ni Samuel Alazar, Yohannes Nega, Essy Kiflom, Yuhannes Tilahun, Merhawi Kesete, Hermon Tecleab, Medhanie Redie, Yosief Ghide, Ahmed Abdurahman, Tesfalem Tekle, Yonatan Solomon, Fitsum Kelati, Mekonen Kibrom, Daniel Alexander, Kuluberhan Gltensae, Merhawi haile, Aman Habteslus na Amir Osman.
No comments:
Post a Comment